FENTHION ICSC: 0655
Septemba 1993

O,O-Dimethyl-O-(4-methylthio-m-tolyl) phosphorothioate
Phosphorothioic acid, O,O-dimethyl O-(3-methyl-4-(methylthio)phenyl) ester
CAS # 55-38-9 C10H15O3PS2/(H3CO)2PS-O-C6H3(CH3)-S-CH3
RTECS # TF9625000 Masi ya molekuli: 278.3
UN # 3018
EC # 015-048-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Degedege. Kizunguzungu. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Msongo/mfiyo (wa jicho) (zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. (zaidi tazama Uvutaji pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 21-25-50/53
S: (1/2-)-36/37-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G45b
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FENTHION ICSC: 0655
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI IWAPO MENYU.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za fosforasi na oksidi sulfuri.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.2 mg/m3 (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1993-1994)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva , kusababisha degedege, kutoweza kupumua. Kizuio cha kolinesterasi. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kizuio cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo =210°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.25
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: kidogo sana
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege, samaki.
VIDOKEZO
Ikiwa katika daraja la kutumika kwa kazi fulani (95-98%) ni mafuta yamiminikayo yenye rangi ya manjano hadi kahawia na harufu inayokaribia ya kitunguu saumu. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Baycid, Baytex, Entex, Lebaycid, Mercaptophos, Queletox na Tiguvon ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005