1,1,1-TRICHLOROETHANE ICSC: 0079
Oktoba 1994

Methyl chloroform
Methyltrichloromethane
alpha-Trichloroethane
CAS # 71-55-6 C2H3Cl3 / CCl3CH3
RTECS # KJ2975000 Masi ya molekuli: 133.4
UN # 2831
EC # 602-013-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka. Tazama Vidokezo. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kusinzia. Kichefuchefu. Upotevu wa mtingiko - kupatana. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. (Zaiditazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 20-59
S: (2-)-24/25-59-61
Angalia: [F]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S2831
Msimbo wa NFPA: H 2; F 1; R 0;
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,1,1-TRICHLOROETHANE ICSC: 0079
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na fosjini na kloridi hidrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na alumini, manganisi na aloi zake, alkali, vioksidishaji vikali, asetoni na zinki. Hushambulia mpira. 1,1,1-trickloroethani na potasiamu au aloi zake hutoa michanganyiko isiohimili mshituko. Kwa taratibu hutendana na maji kutoa asidi hidrokloriki yenye babuzi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 350 ppm kama TWA, 450 ppm kama STEL; A4; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: 200 ppm, 1100 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(1); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri moyo, mfumo mkuu wa neva na ini kusababisha ugonjwa wa moyo na kutoweza kupumua. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 74°C
Kiwango myeyuko: -30°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.34
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 13.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.6
Kiwango cha kumweka: tazama Vidokezo
Jotoridi la kujiwasha: 537°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 8-16
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.49
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa uzuri wa hewa and maji ya ardhini.
VIDOKEZO
Mvuke unaowaka / hewa mahuluti vigumu kuwasha, huweza kupatikana katika hali fulani. The substance burns only in excess oxygen or if a strong source of ignition is present. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Aerothene, Algylen, Trichloran, Chlorylen, Genklene, Chlorothene NU, Chlorothene VG, and Solvent 111 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005