| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Povu linalokinza alkoholi. Poda kavu. Dioksidi kaboni.
|
MLIPUKO |
|
|
|
MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
Ngozi |
Wekundu. Maumivu. Mchomo. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
Kumeza |
Kuumwa koo. Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-III Msimbo wa NFPA : H 2; F 1; R 0; |
| |||||||
|
|
DATA MUHIMU | |||
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU NJANO ISIYOKOZA, KINATACHO, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki MAK haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
Kiwango mchemko: 293-297°C Kiwango myeyuko: 2°C Uzito wiani (maji = 1): 0.95 Umumunyifu katika maji: mbaya Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: <0.01 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.59 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 0,950 Kiwango cha kumweka: 140°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 370°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.28 | ||
DATA YA MAZINGIRA | |||
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye samaki na vyakula vitokavyo baharini.
| |||
VIDOKEZO | |||
Namba nyingine za CAS: 84852-15-3 (mchanganyiko wa isoma).
| |||
MAELEZO YA ZIADA | |||
| |||
| |||
© IPCS, CEC 2005 |