DICHLOROACETYLENE ICSC: 1426
Oktoba 2001

Dichloroethyne
CAS # 7572-29-4 C2Cl2
RTECS # AP1080000 Masi ya molekuli: 94.9
UN #
EC # 602-069-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Kilipukaji. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na asidi au vioksidishaji. Usigusishe na nyuso za moto.
Mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni, USITUMIE podal.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Zima moto ukiwa mahali pa usalama. Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Facial paralysis, numbness. Tetemeko.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Mpeleke kwa daktari. Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha mivuke ya misombo ya kikaboni yenye viwango mchemko vidogo).
Kisichoingiza hewa.
Ainisho ya EU
Ishara: E, Xn
R: 2-40-48/20
S: (2-)36/37
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na asidi kali, na vioksidishaji. Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


DICHLOROACETYLENE ICSC: 1426
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile klorini. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji na pamoja na asidi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (Kiwango cha juu) 0.1 ppm A3 (ACGIH 2001). MAK: Aina ya sarakani: 2 (DFG 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva na mafigo kusababisha vidonda vya tishu, kuharibika kwa utendaji na kuharibika kwa figo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 32°C (kulipuka)
Kiwango myeyuko: -66°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: hakuna
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.3
Kiwango cha kumweka: tazama Vidokezo
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii inaweza kuwaka lakini kiwango mlipuko hakikuelezwa katika maandiko. Mwako katika nafasi funge huenda ukageuka kuwa mpasuko. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dutu hii haipatikani kwa aina ya biashara lakini ni matokeo ya utenganaji la trikloroethilini, trikloroethani na pia kitokezi cha kloridi vinilidini.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001