ISOBUTANE ICSC: 0901
Novemba 1998

2-Methylpropane
1,1-Dimethylethane
Trimethylmethane
(silinda)
CAS # 75-28-5 C4H10 / (CH3)2CHCH3
RTECS # TZ4300000 Masi ya molekuli: 58.1
UN # 1969
EC # 601-004-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizio wa maji.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kukosa pumzi. Msongo wa hewa.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha mivuke ya misombo ya kikaboni yenye viwango mchemko vidogo).
Ainisho ya EU
Alama: F+
R: 12
S: (2-)-9-16
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 501
Msimbo wa NFPA: H 1; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ISOBUTANE ICSC: 0901
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, asetilini, halojeni na oksidi za nitrojeni kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK: 1000 ppm; 2350 mg/m³ IV (1998)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa kusababisha kuharibika kwa utendaji na kutoweza kupumua. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -12°C
Kiwango myeyuko: -160°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.6 (kioevu)
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 304
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 460°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-8.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.8
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Hatua zilizotajwa katika sehemu ya KINGA zinahusu uzalishaji, ujazaji wa silinda, na uhifadhi wa gesi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005