Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

Human rights in China

February 14, 2007

Mwaka elfu mbili na sita umeshuhudia kuendelea kwa tabia ya kukera ya ukiukaji haki za binadam huko China. Wakati huo huo mwaka huo ulishuhudia kuongezeka kwa juhudi za kiufundi na kutangazwa kwenye vyombo vya habari za kundi dogo la mawakili, wasomi wa sheria, wakereketwa wa haki za binadam na waandishi habari, ambao lengo lao ni kupigania haki za kijami na haki za kikatiba kupitia mahakama. Watu hao wanajaribu kufanya kazi kufuatana na mfumo wa kisheria wa China, ili kulinda haki za raia wenzao, wengi wao wamekuwa wahanga wa ulaji rushwa wa maafisa wa serekali.

Jinsi serekali ya China ilivyo jibu kutokana na vuguvugu hilo la kupigania haki, ni la kusikitisha. Wakereketwa wa haki za binadam, waandishi kupitia tovuti, waandishi habari na wasomi wanaendelea kukabiliwa na hatari ya kutiwa vizuizini, kufungiwa nyumbani, kukamatwa na kupatikana na hatia ya uhalifu, mara nyingi kwa misingi yenye masuala yenye shaka. Kitisho cha kubughudhiwa, kupoteza kazi, na ulipizaji kisasi dhidi ya familia za wahusika, kinasababisha uwoga kwa wale amabo huwenda wangelipendelea kueleza malalamiko yao au kufanya kazi katika kulinda haki za raia wenzao.

Moja kati ya kesi mashuhuri inayojulikana ni ile ya Chen Guangcheng, kipofu mkereketwa wa haki za kisheria aliyeorodhesha mateso yanayotokana na sera za China za kuwa na kiwango maalum cha watoto. Alihukumiwa kifungo cha zaidi ya mika mine jela, hapo mwaka 2006 kwa tuhuma zilizokuwa na shaka ya kuzuia usafiri wa magari na kuvunja mali ya uma. Korti ya rufaa iliamrisha kesi yake ifanyiwe upya, lakini hukumu ya awali ya Bw Chen ilipitishwa tena na mahakama ya awali iliyompata na hatia. Utaratibu wote wakati wa kesi yake ya awali, ya marudio na ya kukata rufaa uligubikwa na ukiukaji mkubwa sana wa kutopatiwa haki, ikiwa ni pamoja kushambuliwa kwa mke wa Bw Chen, na tuhuma za kutumia ushahidi wa uwongo.

Marekani, imeeleza malalamiko yake kuhusiana na kesi ya Bw Chen pamoja na ya wengine waloshambuliwa kwa ajili ya kazi zao kwa njia za amani kusaidia haki zao za za wengine. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za njee ya Marekani Tom Casey amesema kwamba Marekani inaihimiza serekali ya China – kama Marekani inavyo wahimiza wengine – “kuheshimu haki za raia wakekutetea kwa njia ya amani haki za raia wenzao. Hakuna mtu yeyote”, alisema Bw Casey, “anabidi kutaabika kwa ajili ya kueleza tu maoni yake, na kwa kutaja wasi wasi wao kuhusiana na sera za serekali.