Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

Freedom of the Press and Iran

February 26, 2007

Kundi la Human Rights Watch, taasisi isiyo ya kiserikali, inatoa tuzo kwa waandishi saba raia wa Iran kwa kutambua kila ilichokiita ushujaa katika kukabiliana na manyanyaso ya kisiasa. Raia hawa wa Iran ni miongoni mwa waandishi 45 kutoka nchi 22 waliopewa tuzi hiyo na Human Rights Watch.

Wale waliopatiwa tuzo hiyo ni pamoja na mwandishi wa habari za uchunguzi, Roozbeh Mir Ebrahimi, alitiwa ndani September 2004 na kushikiliwa kwenye chumba cha peke yake kwa siku 60; mtunzi na mwandishi wa habari, Shahram Rafizadeh, alifungwa mwaka 2004 baada ya kuandika kuhusu jukumu la Mawakala wa upelelezi wa Iran katika mauaji ya waandishi na wapinzani raia wa Iran, na Arasha Sigarchi, aliyefungwa mwaka 2005 kwa kuchapisha habari kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Serikali ya Tehran. Mwingine aliyepewa tuzo ni Ensaf Ali Hedayat, yeye kwa mujibu wa Human Rights Watch, ameripoti kwa kina kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la Azerbaijan nchini Iran. Alikamatwa June 2003 na kuwekwa gerezani katika chumba cha peke yake kwa siku 74. aliachiliwa baada ya kukaa gerezani kwa miezi 18. Bwana Hedayat anasema anafahamu kutokana na kile alichokipitia ni mambo gani wafungwa wa kisiasa wa Iran wanakabiliana nacho nchini Iran.

Nilipotiwa ndani, nilipata fursa ya kuona kile kinachoendelea ndani ya gereza kama mwandishi wa habari. Niliandika siyo tu kile ambacho kimenitokea mimi, siyo tu mateso niliyopata. Niliandika yote ambayo yanaendelea ndani ya magereza ya Iran katika jimbo la Azerbaijan. Niliandika yote kuhusu wafungwa kwa maneno yao wenyewe. Dunia ni lazima ifahamu kitu gani kinaendelea ndani ya Iran, hasa katika magereza kwenye mkoa wa Azerbaijan.

Bwana Hedayat anasema Iran ina magereza mengi mno na wafungwa wengi wa kisiasa.

Kuna magereza 34 yanayotambuliwa rasmi nchini Iran katika jimbo la Azerbaijan. Idadi hii haijumuishi dazeni ya vituo vya vizuizi vya idara ya upelelezi na huduma nyingine za vitengo vya upelelezi. Hakuna anayefahamu vituo hivi viko wapi anasema Bwana Azeri.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Sean Mccormack anasema Marekani inafanya kazi na jumuiya ya kimataifa kupitia Umoja Mataifa, serikali za kigeni na taasisi za kimataifa zisizo za kiserikali kuuangalia utawala wa Iran jinsi unavyoendelea kuwanyanyasa raia wake na kushinikiza kuboresha rekodi yake ya haki za binadamu.