| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
MOTO |
Huungua sana. Kilipukaji.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Maji mengi, mnyunyizio wa maji.
|
MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani. Hatari ya moto na mlipuko inapoyeyuka katika vimumunyishi vya kikaboni.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
Kuvuta pumzi |
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
Ngozi |
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
Macho |
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
Kumeza |
Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu. Degedege.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
|
KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
Shauriana na mtaalam. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru.
|
Ainisho ya EU Alama: E, Xn R: 2-11-20/22-52/53 S: (2-)-39-41-47-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.1 | |||||||
HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
Msimbo wa NFPA: H 3; F -; R 2; Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 41GSR2-S |
Isodhurika kwa moto. Baridi. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
| |||||||
|
|
DATA MUHIMU | |||
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA NYEUPE HATARI KWA MWILI: Iwapo kavu, huweza kuchajiwa kiumemetuamo kwa kuzinga, upitishaji nyumatiki, umiminaji, nk. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana kutokana na kupata joto kuzalisha mafusho yenye sumu kama vile tetramethylsuccinonitrile (tazama ICSC 1121) na sianidi. Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na alkoholi, vioksidishaji, ketoni kama vile asetoni, aldehidi na hidrokaboni kama vile heptani kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri ini. | ||
TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
Uzito wiani: 1.1 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <1 |
Jotoridi la kujiwasha: 64°C | ||
DATA YA MAZINGIRA | |||
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
VIDOKEZO | |||
Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa. Aceto azib, ADZN, AIBN, AIVN, AZDH, CHKHZ, Genitron, Pianofor AN, Porofor N, Porofor-57 na Vazo (64) ni majina ya kibiashara.
| |||
MAELEZO YA ZIADA | |||
| |||
| |||
© IPCS, CEC 2005 |