BORON TRICHLORIDE ICSC: 0616
Oktoba 1997

Boron chloride
Trichloroborane
(silinda)
CAS # 10294-34-5 BCl3
RTECS # ED1925000 Masi ya molekuli: 117.19
UN # 1741
EC # 005-002-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

USITUMIE maji. Moto unapotokea katika eneo: poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi. INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 14-26/28-34
S: (1/2-)-9-26-28-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 8

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BORON TRICHLORIDE ICSC: 0616
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI AU KIOEVU KISICHO RANGI, KIFUKACHO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na maji au hewa yenye unyevunyevu kufanyiza kloridi hidrojeni na asidi boroni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na anilini, fosfini, alkoholi, oksijeni na maunzi kikaboni kama vile grisi au mafuta. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 12.5°C
Kiwango myeyuko: -107°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.35
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 150
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.03
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005