Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

Human Trafficking In China

March 29, 2006

Biashara ya kusafirisha na kuuza binaadamu ni utumwa wa miaka hii ya sasa ambao hutumia utekaji nyara, wizi, vitendo dhidi ya akili za mtu na vitendo vya utumiaji nguvu kuwalazimisha wanaume, wanawake na watoto kufanya kazi bila ya hiari yao na kutumiwa kwa vitendo vya ngono. Inakadiriwa watu mia nane elfu wanasafirishwa na kuuzwa kuvuka mipaka ya kimataifa kila mwaka.

Nchini China, kama vile katika nchi nyingi za Asia, Wanawake wa Kichina na wasichana wanachukuliwa na wafanyabiashara haramu ya kusafirisha na kuuza binaadamu ambao wanawasafirisha wanawake na wasichana nchi za nje kwenda kutumiwa kwa ngono. Walchina wanaume kwa wanawake wanaihama nchi yao na kwenda kote duniani kutafuta kazi za vibarua zenye kuhitaji ujuzi mdogo na idadi kubwa miongoni mwao wanakabiliwa na vitendo vya kulazimishwa kufanya kazi bila hiari yao, bila malipo. Kuna ripoti pia za wafanyakazi wahamaji kulazimishwa kufanya kazi ndani ya China yenyewe.

Ingawaje serikali ya China inasema kwamba inapinga vikali biashara ya kusafirisha na kuuza binaadamu na imepitisha sheria kuifanya biashara hiyo kuwa si halali, hatua zaidi zinahitajika kuzuia usafirishaji wa binaadamu na kuwalinda wahanga wa biashara hiyo. Wahanga wa biashara hiyo nchini china, hasa wanawake na watoto wanapaswa kuelimishwa kwamba, ahadi za kazi nzuri nchi za nje zinaweza kuwa mitego ya hatari kwao.

Marekani imeisihi serikali ya china iongeze juhudi zake za kutawanya habari kuhusu hatari ya biashara ya usafirishaji na uuzaji wa binaadamu kwa wananchi wake wengi ambao wanavutiwa na uwezekano wa kwenda kufanyakazi nje ya nchi. Marekanii vile vile, imerudia kuisihi serikali ya China iheshimu uhuru wa kupashana habari kama njia moja ya kuelimisha raia wake juu ya hatari za biashara haramu ya kusafirisha na kuuza binaadamu.

Serikali ya China kwa ushirikiano na Shirikisho la kazi Duniani imechukuwa hatua za kuzuia watu kulazimishwa kufanya kazi katika majimbo tisa ya China. Serikali ya China imetowa mafunzo pia ya kuelimisha maafisa wa vyombo vya dola juu ya biashara haramu ya kusafirisha na kuuza watu. Lakini bado hatua zaidi zinahitaji kufanywa.

Marekani ina nia ya dhati ya kuzisaidia nchi zote duniani kukomkesha biashara haramu ya usafirishaji na uuzaji wa binaadamu. Tangu mwaka elfu mbili na moja, Marekani imechanga kiasi cha dola mia tatu na sabiini na tano milioni kusaidia mipango ya kupambana na biashara haramu ya usafirishaji na uuzaji wa binaadamu. Juhudi hizi zimezaa matunda. Mwaka elfu mbili na nne, wafanyabiashara elfu tatu wa biashara haramu ya usafirishaji na uuzaji wa binaadamu walipatikana na hatia mahakamani duniani kote na nchi thelathini na tisa za dunia zilifanya marekebisho au zilipitisha sheria mpya za kupambana na biashara haramu ya usafirishaji na uuzaji wa binaadamu.

Rais wa Marekani, George W. Bush alieleza vizuri sana aliposema kwamba, “Tunavutwa na kuitwa na hisia zetu za huruma kukomesha kabisa vitendo hivi vya kikatili.”