Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial 2006

Tsunami Anniversary

Januari 09, 2006

Tangu mwaka jana kulipotokea mawimbi makubwa ya tsunami yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi chini ya bahari na kuathiri nchi kumi na mbili kusini mashariki mwa Asia, Marekani imetowa zaidi ya dola milioni mia nane arobaini za misaada. Kufuatana na kituo cha ufadhili na uhisani katika chuo kikuu cha Indiana hapa Marekani, watowaji michango binafsi nchini Marekani wamechanga fedha nyingine zaidi - dola bilioni moja na mia nane milioni. Raia wa nchi nyingine nyingi walitowa misaada pia. Rais wa marekani George W. Bush alisema kwamba, Dunia iliungana kusaidia katika jana hilo la dharura:

Rais Bush alisema, marekani inapeleka chakula, dawa, na misaada mingine muhimu katika eneo hiilo la Kusini mashariki mwa Asia. Alisema, marekani inazingatia juhudi zake katika kusaidia wanawake na watoto ambao wanahitaji misaada maaluimu pamoja nayo, ulinzi dhidi ya biashara dhalimu ya binaadamu kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Nchini Indonesia, ambako watu wapatao mia moja sitini elfu walikufa Desemba 26 ilipotokea Tsunami, misaada iliyotolewa na Marekani ni pamoja na masikani ya muda, chakula, mitambo ya kuchuja na kusafisha maji. Barabara kubwa iliyoharibiwa vibaya ambayo inaunganisha Banda Aceh na mji wa Meulaboh inajengwa upya.

Nchini Sri Lanka, mipango ya Marekani ilitowa mambo ya usafi na vifaa vya nyumbani kwa waathiriwa wa Tsunami, ilitowa chakula na usafiri kwa wafanyakazi wa mipango ya dharura ya kulisha watu, iliwaajiri wananchi kufanya kazi ya kusafisha miji baada ya Tsunami kupita, na ilitowa masikani ya muda ambayo imewasaidia zaidi ya waathiriwa elfu hamsini. Marekani vile vile ilijenga tena shule na hospitali, ilitowa misaada ya fedha na mikopo kwa wafanyabiashara, na ilisaidia wavuvi na vifaa vya kuvulia samaki kwa wavuvi zaidi ya elfu tatu.

Katika visiwa vya Maldive, Marekani ilitowa vifaa vya masikani ya muda, ilitowa maji safi, na ilifanya marekebisho kwa bandari na njia na mifereji ya kupitishia uchafu. Nchini Thailand, marekani ilinunuwa boti mpya ishirini za kuvulia samaki na ilitowa mikopo na mafunzo kuwasaidia watu kuendesha maisha yao upya katika biashara ndogo ndogo na uvuvi wa samaki. Misaada pia ilitolewa kwa Malaysia, Somalia, India, na Ushelisheli. Vile vile katika eneo hilo, marekani inaweka mitambo yenye kutowa onyo la awali pale inapotokea mitetemeko baharini na Tsunami kwa ushirikiano na tume ya kimataifa inayoshughulikia bahari chini ya shirika la UNESCO lililopo chini ya umoja wa mataifa.

Kama alivyosema rais Bush, Marekani inania ya dhati ya kusaidia watu wanaoteseka. Alisema, marekani imenuia leo na itanuia kesho.