NITRIC ACID ICSC: 0183
Aprili 1994

Concentrated Nitric Acid (70%)
CAS # 7697-37-2 HNO3
RTECS # QU5775000 Masi ya molekuli: 63.0
UN # 2031
EC # 007-004-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na maunzi vinavyoweza kuwaka au kikaboni.
Moto unapotokea katika eneo: USITUMIE povu.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na misombo ya kawaida ya oganiki.

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Inababua. Mibabuko ya ngozi nzito. Maumivu. Kubadilika kuwa njano.
Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Inababua. Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Inababua. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Katisha salio kwa uangalifu kwa kabonati natiri. Kisha osha kwa maji mengi. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: O, C
R: 8-35
S: (1/2-)-23-26-36-45
Angalia: [B]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) -TEC (R)-80S2031-II au 80GO1-I
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0; OX
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, besi, vyakula na malisho, maunzi kikaboni. Baridi. Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NITRIC ACID ICSC: 0183
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapopata joto huzalisha oksidi nitrojeni. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayowaka na yanayonakisi, mfano, tapentaini, mkaa, alkoholi. Dutu hii ni asidi kali, humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji kwa metali. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na misombo kikaboni (kama vile asetoni, asidi asetiki, anhidridi asetiki), kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia baadhi ya plastiki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm kama TWA, 4 ppm kama STEL; (ACGIH 2004).
MAK: 2 ppm, 5.2 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kali kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo).

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 121°C
Kiwango myeyuko: -41.6°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.4
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 6.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.07
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya saa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Namba nyingine ya UN 2031 asidi nitriki zaidi 70% , ainisho ya hatari 8, jasara tanzu ya UN 5.1 kikundi ufungashaji I.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005