CARBON BLACK ICSC: 0471
Machi 1995

CAS # 1333-86-4 C
RTECS # FF5800000 Masi ya atomi: 12.01
UN # 1361 (kaboni ya kiasili ya mnyama au mimea)
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 42GS2-II+III
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CARBON BLACK ICSC: 0471
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
VIDONGE NYEUSI AU PODA NYOVU KUZIDI KIAZI. ISO HARUFU

HATARI KWA MWILI:
Vumbi nyingi yaweza kuwaka moto ikiguza nyuso kuna joto chingi (zaidi ya 500°C).

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza gesi zenye sumu sana (monoksidi kaboni ICSC 0023). Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali kama vile klorati, bromati na nitrati.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 3.5 mg/m³ kama TWA; A4; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa kikoleza cha juu. (Tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: takribani 3550°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.8-2.1
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Aina zingine za kaboni nyeusi huwa na ambatani inayozababisha sarakani na sehemu ya hizi imeloanishwa kama inayoweza kusababisha sarakani kwa binadamu. Uangalifu mkali lazima uwepo ili kuzuia kugusa. Athari kwa mapafu haijaamuliwa na huenda ikawa kwa sababu ya mchanganyiko. Huenda ikawa kwamba athari iliyoko ni kwa sababu ya kugusa kwa kawaida kwa vumbi ya kawaida. Poliaromatiki haidrokaboni (PAH) imeshaonekana kwa kaboni nyeusi. Kwa kutegemea njia ya kutengenezaji kuna aina nyingine ya kemikali. Kaboni nyeusi hua na asili mia nane ya mvuke (<8%) na inaweza kusababisha mlipuko. Kaboni nyeusi ya madini haina namba ya UN na haijaloanishwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005