ANTHRANILIC ACID ICSC: 1295
Novemba 1998

2-Aminobenzoic acid
Carboxyaniline
1-Amino-2-carboxybenzene
CAS # 118-92-3 C7H7NO2
RTECS # CB2450000 Masi ya molekuli: 137.1
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 1; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ANTHRANILIC ACID ICSC: 1295
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MAGAMBA ISO RANGI HADI MANJANO AU PODA FUWELE NYEUPE HADI MANJANO, ISO HARUFU

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza monoksidi kaboni, oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 146-148°C
Uzito wiani: 1.4 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.6
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 52.6°C: 0.1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.73
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0
Kiwango cha kumweka: 150°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.99-1.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege.
VIDOKEZO
Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Vitamin L ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005