SULFOTEP ICSC: 0985
Oktoba 1999

Thiodiphosphoric acid tetraethyl ester
Ethyl thiopyrophosphate
Tetraethyl dithiopyrophosphate (TEDP)
CAS # 3689-24-5 C8H20O5P2S2 / (C2H5O)2-P(S)-O-P(S)-(OC2H5)2
RTECS # XN4375000 Masi ya molekuli: 322.30
UN # 1704
EC # 015-027-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Kiwekeo kinaweza kulipuka kwa ukali sana kwenye joto la moto.

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Degedege. Kupoteza fahamu. Udhaifu. (Tazama Kumeza).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Kutokwa na jasho na kutetemeka mahali pa ufyonyaji. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Msongo/mfinyo wa jicho.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Kuchanganyikiwa. Kuhara. Kutapika. Kupungua hamu ya kula. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 27/28
S: (1/2-)-23-28-36/37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kavu. Kilichofungwa vizuri. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Usihifadhi kwenye vyombo vya metali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SULFOTEP ICSC: 0985
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANOISIYOKOZA, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu sana (oksidi za fosforasi na oksidi za sulfuri). Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia chuma, aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.2 mg/m³ (ngozi A4) (ACGIH 1999).
0.1 mg/m³ ngozi EC OEL
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, kusababisha degedege, kutoweza kupumua. Kizuizi cha kolinesterasi. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kizuizi cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 0.2666kPa: 136-139°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.0226
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.99
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Zao la kiteknikali ni kioevu rangi ya iliyokolea, kiwango mchemko 131-132°C ifikapo 0.267 kPa. Usichukue nguo za kazi nyumbani. ASP 47, Bay-E-393, Bladafum, Dithion, Dithiotep, Dithiofos ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005