1-HEXADECANETHIOL ICSC: 0025
Aprili 2004

Hexadecyl mercaptan
1-Mercaptohexadecane
Cetyl mercaptan
Hexadecane-1-thiol
CAS # 2917-26-2 CH3(CH2)15SH / C16H34S
RTECS # Masi ya molekuli: 258.5
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Povu, dioksidi kaboni, poda.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kusanya salio kwa uangalifu,
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, kinakisishaji, metali, asidi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1-HEXADECANETHIOL ICSC: 0025
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu pamoja na oksidi za sulfuri. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, asidi, kinakisishaji, metali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 0.93kPa: 184°C
Kiwango myeyuko: 18°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.84
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 10
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 8.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 135°C o.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kiwango cha joto cha kuweza kuwaka yenyewe havipo katika maandiko. Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005