SILVA ICSC: 0810
Oktoba 1997

Argentium
C.I. 77820
CAS # 7440-22-4 Ag
RTECS # VW3500000 Masi ya atomi: 107.9
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki isipokuwa ikiwa poda: vumbi huwaka.


MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na amonia, mimumunyo mikali ya peroksidi hidrojeni, asidi kali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SILVA ICSC: 0810
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
METALI NYEUPE, HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA OZONI, SULFIDI HIDROJENI AU SULFURI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa asetilini. Humenyuka pamoja na asidi kusababisha athari ya moto. Mgusano na mmumunyo wa peroksidi hidrojeni kali yaweza kutengana kwa nguvu kutoa gesi ya oksijeni. Mgusano na amonia waweza kutoa misombo lipukaji ikiwa mikavu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (metali): 0.1 mg/m3 (ACGIH 1997)
MAK: 0.1 mg/m3 (1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kuvuta pumzi ya mvuke wa silva wa viwango vya juu kunaweza kusababisha uharibifu wa mapafu na uvimbe wa mapafu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kutoweka kwa rangi kijivu-bluu kwenye macho, pua, koo na ngozi (argyria/argyrosis).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 2212°C
Kiwango myeyuko: 962°C
Uzito wiani (maji = 1): 10.5
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005