UNABII WA 120

 

 

 

Usikate Tamaa! Usikubali Kushindwa! Unabii wa Marejesho ya Sukkot Kwa Mfasiri wa Kiebrania, Wayahudi wa Kimasihi na Waumini Wote

 

Ilipokewa Oktoba 19, 2011

 

 

 

YAHUVEH alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabiii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY inayovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

 

                         *******

 

Unabii huu una upako wa marejesho, nguvu, ujasiri, kwa hivyo kama unahisi uchovu wa kupigana vita na umechoka mwache YAHUSHUA akunawirishe wakati huu wa Sukkot na Unabii wa Marejesho kwa wale wote wanaomwabudu YAHUSHUA na wanaoishi kwa Utakatifu.

 

 

 

Hii itarejesha wengi wa wale wanajeshi ambao wamepata vipigo. Imani ya wanajeshi inafaa kujengwa. Hakuna kuvumiliana kule Israeli kwa wale wanaomwamini na kumfuata YAHUSHUA. Elisabeth asema, “Ilimchukua Myahudi aliyeteswa kukoroga upako ndani mwa huyu Myahudi aliyeteswa.” Kama umechoka na umepata vipigo, tafadhali soma na usikize. Kuna upako wa marejesho hapa. Kuna upako mkubwa zaidi katika Neno linalozungumzwa. Tafadhali sikiza rekodi ya kinaza sauti katika video au isome kwa sauti kubwa kama unaweza.

 

 

Tafadhali angalia pale mwisho, kulitokea miujiza na kinaza sauti. Betri ilikuwa na nguvu ya kutosha tu kunaza urefu wa Neno yenyewe pekee. Kama mazungumzo ya simu yangekuwa yamenazwa kutoka mwanzoni, Neno lote halingekuwa limenazwa mpaka mwisho. Lakini Sifa iwe kwa YAHUSHUA, sauti ilianza kunazwa kwa wakati kamili wa YAHUVEH na Neno lote lilinazwa!

 

 

Unabii Wa Sukkot Wa 120 Kwa Mfasiri Wa Kiebrania

 

 

Usikate Tamaa! Usikubali Kushindwa! Unabii wa Marejesho ya Sukkot Kwa Mfasiri wa Kiebrania, Wayahudi Wa Kimasihi na Waumini Wote

 

 

Ilipokewa Oktoba 19, 2011

 

Siku ya 6 ya Sukkot – kalenda ya kuangalia Mwezi Mwandamo Mpya

 

 

Kinaza chaanza hapa.

 

Elisabeth: … miguu yako. Nataka kurudia haya. Naona miguu yako. Na YAHUSHUA asema kila mahali unapokanyaga, kwenye nyayo za viatu vyako, kwenye nyayo za miguu yako, ipo damu yake YAHUSHUA kwa kuwa unafuata katika nyayo zake. Yeye hutembea katika viatu vyako na upako wa RUACH HaKODESH ipo juu yenu. Ipo kwenye nyuso zenu. Ipo ndani ya macho yenu. 

 

 

Neno linaanza:

 

Wanipendeza mwana WANGU. Usiogope kuniita mimi MWENYEZI MUNGU

BABA kwa kuwa, ROHO YANGU ipo ndani yako. Wewe ni WANGU! Wewe umeoshwa na damu! Wewe umenunuliwa na damu! Na wewe ni WANGU: akili, mwili, roho na moyo ni mali yake YAHUSHUA ha MASHIACH! MIMI NDIYE MASIHI wako! ([Elisabeth:] “O nahisi joto!”) Na sasa Ninakujaza na mafuta mapya kutoka mbinguni ya kutembea katika upako mkuu zaidi wa kuongea kwa ujasiri mkuu, kama Yohana Mbatizaji. Kutoka taji la kichwa chako hadi nyayo za miguu yako! Manna kutoka mbinguni, nakupa ule!

 

 

 

Wewe ni Mpendwa WANGU! Mpendwa WANGU ni WANGU! Oh ewe Mpendwa WANGU! NISAIDIE, NISAIDIE, NISAIDIE! Lisha Kondoo na Wana Kondoo WANGU! Fanya kazi karibu na Nabii huyu, kwa kuwa muda ni mfupi sana!

 

 

 

 

Damu yangu imeloweka kwenye udongo kule Israeli. Tone moja tu inaweza kuosha dhambi. Asante kwa kuwa huoni aibu kwa kunijua MIMI. Asante kwa kuwa tayari kuteswa kwa ajili YANGU. Asante kwa kunikubali MIMI, hata kama inamaanisha familia yako watakugeuka! Wale wa familia yako kwa damu, lakini si familia YANGU kwa Damu. Familia YANGU kwa Damu wanakukumbatia kama vile Nilivyomwagiza huyu nabii aliye dada yenu kuwaita siku hii! Familia YANGU kwa Damu, wale ambao hutenda matakwa ya BABA aliye Mbinguni, wanakukumbatia na wanakupenda, wanakutambua kwa kuwa wewe uko ndani YANGU! Kumbuka haya daima!

 

 

 

Ninakupenda! Na ninakupa asante! Ndio, MUNGU BABA wako, BWANA wako, MASIHI wako, anakupenda! Usiwahi, usiwahi, usiwahi, usiwahi acha yeyote achukue haya kutoka kwako! MIMI hukuongelesha katika utulivu wa usiku. Ninakupa funuo. Na funuo kubwa zaidi utapata! Kumbuka mpendwa WANGU, Yuda watakuja na Yuda watakwenda. Nilikuwa na Yuda WANGU. Wewe una wako. Elisabeth ana wake. Wote, wote, wote wanaofuata nyuma YANGU, wasipoteswa katika Jina LANGU, wanapaswa kujiuliza, “Kwa nini?” kwa kuwa mtumishi sio mkubwa kushinda BWANA. Ni wote… Wote hawanipendi MIMI. [Yaani, Sio wote wanaonipenda]. Usitarajie wote wakupende­­­­­­­­­­­ ­­­­- kwa vile bado Ninateswa. Katika ulimwengu huu Ninachukiwa zaidi ya kupendwa! Ninakejeliwa zaidi ya kukubaliwa! Lakini nililipa gharama pale Kalvari na Israeli, O Israeli kwa muda gani, muda gani, muda gani, muda gani  lazima Nisubiri ili mnikubali MIMI, mnipende MIMI?

 

 

 

O Ninajua ni muda gani utakuwa! Na Ninajua ni gharama gani Israeli italipa! Na itakuwa gharama nzito sana - kwa kuwa watawajibika zaidi - kwa kuwa nilitembea kwenye mitaa ya Yerusalemu. Damu YANGU, Damu YANGU, Damu YANGU imeloweka katika ardhi hiyo. O, vile Ninavyohuzunika, vile Ninavyoomboleza! Lakini kuna mabaki! MIMI nina mabaki! DAIMA MIMI huwa na mabaki. Wako wachache - lakini ni WANGU! Na kama vile tu nina wewe, kwa hivyo pia kuna wengine walio Israeli. Na wako kote ulimwenguni na watasimama na watatetea! Na wanatetea yote yaliyo Takatifu! Na wanafichua na kukemea yote ambayo sio Takatifu na wanaonya kuwa masihi bandia yupo njiani - lakini haitakuja kupita mpaka nimemchukua Bibi Arusi WANGU wa ukweli.

 

 

Kwa hivyo ninachukua muda huu kusema “Asante!” Ninamtuma Nabii huyu WANGU kusema, “Asante.” Hamna hata chozi moja lililomwagwa, kama imefanyika kwa ajili ya Jina LANGU, ambalo halijahifadhiwa kule juu Mbinguni katika chupa cha dhamana kuu, iliyozungukwa kote na johari za kila aina. Na mateso yakiwa makuu zaidi - Ninawaambia hivi Wapendwa WANGU, Bibi Arusi WANGU Mpendwa - ndio harufu huwa na nguvu tena zaidi, manukato iliyo kwenye hiyo chupa ya machozi yako. Imekuwa dhabihu KWANGU, YAHUSHUA wako, BABA yako aliye Mbinguni na RUACH ha KODESH Mpendwa.

 

 

O ni kwa muda gani, kwa muda gani, kwa muda gani, kwa muda gani, kwa muda gani, kwa muda gani Nimesubiri ili niweze kumkumbatia Bibi Arusi WANGU! Lakini haitakuwa muda mrefu sana! Haitakuwa muda mrefu sana! Utakuwa katika mikono YANGU! Utasikia sauti YANGU! Usikate tamaa hata! Usikubali kushindwa! Kwa sababu umetoka mbali mpaka sasa! Usikate tamaa! Usikubali kushindwa! Usiafikiane na uongo wa dunia! Ulimwengu ukizidi kukuambia kuwa wewe sio mtakatifu, jua ya kuwa wewe ni Mtakatifu! Wakizidi kukukejeli na kukucheka kwa sababu unafuata Sheria ya Torati, jua ya kwamba wewe ni WANGU!

 

 

Ukizidi kutetea Sabato, Shabbat, na kusema, “Sio Jumamosi”, jua tu kuwa wewe ni WANGU! Usikate tamaa! Usikubali kushindwa! Ingawa  mateso ni mazito zaidi na ingawa yatazidi kuwa mazito, kumbuka ni katika Jina la nani unateswa! Kumbuka ni kwa ajili ya nani unachukiwa!

 

O watatumia jina lako na jina lako watalitukana na kusema kila namna ya uovu dhidi lake, lakini sio jina lako ambalo wanalolichukia. Ni yule ambaye unayemwakilisha. Ni wewe ulivyo katika MIMI. Ni Jumbe ambazo unawapa zinazotoka Mbinguni.

 

Kwa hivyo usikate tamaa! Usikubali kushindwa! Kwa sababu nitalipisha kisasi kwa hawa maadui! Na wataomba milima ziwafiche -kuepuka YULE anayeketi kwenye Kiti cha Enzi! Na MWANA KONDOO Mtakatifu aliyechinjwa, sulubiwa na kufufuka! Jina LANGU ni YAHUSHUA ha MASHIACH! Na Ninakuambia usikate tamaa! Na usikubali kushindwa kwa sababu MIMI niko pamoja nawe!

 

Wafikie watu WANGU. Wafikie watu WANGU. Sizungumzi bali tu na watu walio Israeli, lakini Ninazungumza na watu wote ulimwenguni. Wafikie watu WANGU.

 

 

 

Endelea kuwalisha Kondoo na Wana Kondoo. Endelea kutoona aibu kwa ushuhuda wako kwa kuwa ushuhuda wako sio wewe ulivyo, ushuhuda wako ni MIMI nilivyo - ndani yako! Hili ndilo jambo shetani huchukia. Hili ndilo maadui wako huchukia!

 

 

 

Lakini ushuhuda huu wenyewe unaonyesha kweli MIMI ni nani - kwa kuwa MIMI hubadilisha maisha! Na kubwa, kubwa, kubwa, kubwa, kubwa, kubwa, kubwa ni zawadi zilizo Mbinguni kwa wale ambao wamekuwa tayari, tayari kuweka chini sifa zao, majina yao, wamekuwa tayari kuteswa kwa ajili ya Jina LANGU! Kubwa, kubwa, kubwa, kubwa, kubwa ndizo zawadi zinazowangojea Mbinguni.

 

 

Mtaona enyi Wapendwa Wangu, mtaona

Utukufu WANGU, Utukufu WANGU, Utukufu WANGU. Na macho yenu, mtaona. Sio mbali sana. Msikate tamaa mkiwaona wanaotunga tarehe bandia wakija na kuenda. Sikiza tu na utaona. Funuo mpya zitakuja kwako.

 

Simameni kwa niaba ya wengine. Sasa sio wakati wa kusimama pekee yako. Naleta Bibi Arusi WANGU pamoja kutoka mwisho mmoja hadi mwingine ulimwenguni kupitia mtandao huu! Bila hivyo, nyinyi wawili mnaozungumza hamngekuwa mmekutana. Na bado, ni kama mko katika chumba kimoja kwa kuwa nyinyi ni Roho moja.

 

 

Mtajua ni nani walio WANGU. Watapigana karibu nanyi. Watasimamia yote yaliyo Takatifu. Watawafichua wale mbwa mwitu wanaovalia ngozi ya kondoo. Msidanganyike. Wote ambao husema kuwa wanaongea katika Jina la Yesu Kristo sio wote kwa kweli wanongea juu YANGU. Yeyote anayesimama dhidi ya Huduma hii Takatifu, Huduma iliyokadiriwa na YAH… Ole wao maadui wanaosimama dhidi ya yote yaliyo Takatifu - kwa kuwa unasimama dhidi ya MWENYEZI MUNGU.

 

Kwa hivyo Wapendwa WANGU, jueni ya kwamba Nimewachagua. Jua ya kwamba wewe ndiye Mfasiri wa Kiebrania na bado kuna wengi wanaokuja lakini wamechelewa. Kwa hivyo hii ndio zawadi yako leo. Ulitaka Neno. Umepata Neno.

 

 

 

Elisabeth ulisema, “Sijui nitasema nini!” Huo ni ukweli binti YANGU, kwa sababu haya sio maneno yanayotoka kwenye nyama yako! Haya ni Maneno yanayotoka Mbinguni - kumbariki mfasiri wa Kiebrania atakayechukua Maneno YANGU kwa watu Waebrania na kufanya kazi kwa makini. Na nitambariki [mfasiri] sana!

 

Ninakupenda! Ninakupenda! Usiwahi sahau, kamwe, kamwe, kamwe, kamwe kuwa MIMI Ninakupenda! Ninajua kila chozi uliyomwaga! Ninajua kila moja ya wakati jina lako limelaaniwa katika dunia hii lakini sio kutoka KWANGU, kwa kuwa MIMI hutuma baraka kwako!

 

Ninatayarisha meza mbele yako, mbele ya maadui wako na MIMI NAKUBARIKI WEWE!!! Na Jehanamu yote INAKASIRIKA kwa sababu hawawezi kunyamazisha sauti ya MWENYEZI YAHUVEH wako, ANAYEISHI! Kwa hivyo saga meno yenu kwa hasira!!! Mimi sio yule Mwana Kondoo wa dhabihu anayeteswa tena! Hiyo ilikuwa mara moja tu! Sasa MIMI ni SIMBA kutoka Kabila ya YUDA na Naja kuwameza maadui WANGU!!!!! Kwa kuwa MIMI na BABA ni kitu KIMOJA! SISI tunabariki na pia SISI tunaweka laana! Kumbukumbu la Torati 28, baraka na laana: Baraka ni za wale WANAOTII! Laana ni za wale wasiotii!

 

 

Unatembea katika Baraka ZANGU. Wale wanaofanya matakwa ya BABA aliye MBINGUNI wanatembea katika Baraka ZANGU. Ninawajaribu. Tayari Ninajua ni nani anafaa kuepuka Dhiki Kuu. Nyote mnajaribiwa! Sasa una Unabii mpya Elisabeth Elijah. Umesubiri na umesubiri na maadui waliogopa lakini Nilisubiri na Nilisubiri mpaka sauti hii ulipoisikia - ya mfasiri wa Kiebrania -  kukoroga upako ndani yako.

 

 

Lakini Israeli, Ninakupenda. Je, Mnanisikia MIMI O Israeli? Ninakupenda. Nina hamu ya kukuokoa. Ni chaguo lako. Itachukua mateso, kama huyu unayezungumza [Elisabeth] naye sasa, ameteswa na wengi wao pia. Lakini nina Bibi Arusi WANGU Israeli. Wao ndio Bibi Arusi waliofichwa. Hamna tu Israeli ya kimwili - kuna Israeli ya kiroho. Na nina Bibi Arusi WANGU. Kwa kuwa Israeli WANGU wa kiroho wapo katika Israeli pia.

 

O azizi ZANGU! Someni Kitabu cha Wimbo wa Solomoni. Ona mapenzi YANGU kwenu. Ona mapenzi YANGU kwa Bibi Arusi WANGU. Hujui ni kwa hamu gani Ninataka kuwachukua muwe karibu na MIMI! Na haitakuwa muda mrefu sana! Kwa kweli haitakuwa muda mrefu sana! Ninaona machozi yenu. Ninasikia huzuni wenu. Ninatazama mkilia na kuomboleza, “Mimi sitaki kuendelea kuishi duniani humu.”

 

 

 

Mmezungukwa na uovu katika kila upande.

Lakini unafikiria MIMI huhisi vipi wakati Jina LANGU linapochukiwa? Haitakuwa muda mrefu sana! Usikate tamaa! Usikubali kushindwa! Ile kazi mzuri niliyoianza, Nitaimaliza.

 

 

Mwisho wa Neno.

 

Elisabeth: HalleluYAH! YAHUSHUA Asifiwe! Ndio! [KICHEKO cha furaha] O BABA YAHUVEH, YAHUSHUA, RUACH ha KODESH Mpendwa, Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Kila mtu alisubiri na kila mtu alisema, “Elisabeth, imekuwa muda mrefu tangu kumekuwa na Unabii mwingine. Wapi Unabii? Umekuwa na Unabii zilizohifadhiwa.”

 

 

 

 

Lakini BABA YAHUVEH katika jina la YAHUSHUA, tunakupa shukrani na tunatoa sifa KWAKO saa uu huu! Huu ndio Unabii unaofuata na ilimchukua Mwebrania kutoka Israeli kuiacha huru, katika jina la YAHUSHUA ha MASHIACH! HalleluYAH! O Nahisi joto! Sifa iwe KWAKO YAHUSHUA! Woohoo! Ni nini unasema mpenzi? (Mume wangu ananionyesha kitu).

Sijui ni nini inachosema, inasema nini?

 

 

 

Niko: Betri inamulika ya kwamba imekufa.

 

[Mazungumzo yanaendelea kama haisikiki kamili, kwa muda kidogo kabla ya betri kufa kabisa].

 

 

Elisabeth: Kuna chochote…?

 

Niko: Bado - Namaanisha…

 

Elisabeth: Oh Sawa, betri inamulika kuwa imekufa - lakini HalleluYAH! Tumeipata kwenye kaseti, au sio mpenzi?

 

Niko: Nafikiri…

 

Elisabeth: Tuhakikishe ujumbe upo hapo… O tafadhali MWENYEZI MUNGU...

 

Rekodi Inaisha Hapa.

 

Imezungumzwa kupitia chombo cha udongo, lakini shujaa hodari wa YAHUSHUA. Kwa hivyo imezungumzwa, kwa hivyo imeandikwa katika siku hii ya Oktoba 19, 2011 masaa ya usiku wa manane katika siku ya 6 ya Sukkot kulingana na kalenda ya kuangalia Mwezi Mwandamo Mpya.

 

 

Contact AmightyWind