Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]        Rudi Table

 

 

[ASMA - Urafiki Jazz] 

(Chini ya uongozi wa Juma Mrisho ( NGULIMBA WA NGULIMBA))

Safari yetu ndefu aaah,

Mimi na wewe,

Asma mpenzi ooh wa moyo wangu,

Kiu ya mapenzi imetupata

Mimi na wewe,

Tumuombe Mola atulinde tuwe salama.

Tumezungurukwa na majaribu

Mengi sana,na tujitahidi kuyakabili tuwe salama

Tukishaokoka,Mola wetu , atuweke salama!!!

Kibwagizo:

Asma,ooh Asma ( wa moyo)

Wewe ndiwe uliye rohoni mwangu ( Asma )

Nakuomba ushike maneno haya,

( Kweli mwana )

Ili mapenzi yetu yafanikiwe,

Tukijaliwa tupate funga ndoa yetu,

Oooh Asma, ooh Asma wa moyo

Asma , ooh Asma ...

[Rudi mwanzo]

 

[Jembe Na Panga (Gezaulole) - Urafiki Jazz Band]

 

[Wote]

Baba na mama, Shangazi na Mjomba

Mji hautufai twendeni Gezaulole!

 

Biashara ya Kahawa na maji ya Barafu

Sasa haitufai twendeni Kibugumo

 

Songasonga na kijiji, Tegeta na Mwanadilatu

Haya hasa ndio makao ya mwana wa Mapinduzi

 

Kitambulisho cha Gezaulole ni Jembe na Panga lako!

Hiyo ndiyo Certificate ya mtu mwenye busara

 

(Chorus)

 

[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee

[Mmoja]Biashara ya Njugu na Korosho sasa haitufai eee

[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee

[Mmoja]Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya

[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee

[Mmoja]Gezaulole baba hoo, Gezaulole mama twende

[Wote]Gezaulole baba, Gezaulole mama ee

[Mmoja]Twende eee..........

[Rudi mwanzo]

 

[Kosa Ni La Nani - Urafiki Jazz Band]

 

Wazee nimekuja kumshtaki mume wangu,
Amerudi kazini saa sita,
Njaa yamuuma,  
Kaniuliza chakula nikamwambia bado
 
 
Mara akaingia jikoni ,
Akaanza kupika,
Lakini bahati mbaya mikono ikaungua
 
Mume kashika mikwaju kaanza kunitandika
Kosa la nani eeeeeh  ?

 

(Chorus)

 

[Wote]

Mume wangu baaba ana tabia mbaya sana

Kila nikianza kupika hunifuata jikoni

 

[Njemba wa Bakora]

Muongo sana mke wangu muongo haa

Sina tabia kama hiyo wazee ee

Hivyo ni visa vya mke wangu amezowea kugombana

Tena huchelewa kupika muongo haa

 

[Wote]

Mume wangu baaba ana tabia mbaya sana........

 

Rudi mwanzo

 

 

[Kwa Mjomba - Urafiki Jazz Band]
 
[Wote]
 
Nilipokwenda kwa Mjomba, Nilikutana na binamu yangu
 
Na kwa kweli, Tulipendana
 
Wazazi wetu walitukatalia tusioane
 
Eti kwa sababu, Yeye ni mtoto wa Mjomba
 
Ndivyo ilivyokuwa vigumu kwetu kufunga ndoa
 
(Chorus)
 
[Wote]
 
Wazazi ninasema....nasononeka!
 
Kwa vile msichana....nilimpenda
 
[Mmoja]
 
Basi mwanangu nakuomba usikitike sana
 
Tuliza roho dunia hii ni pana sana kijana
 
[Wote]
 
Wazazi ninasema....nasononeka!
 
[Mmoja]
 
Utampata wako mwingine pia utampenda
 
Mtoto wa mjomba kweli kuoana si vizuri
 
 [Wote]
 
Wazazi ninasema....nasononeka!...........

Rudi mwanzo

 

[Sara(Wacha Majivuno) - Bendi]

 

Heeee Sara wacha majivuno ee

Usiwe kama Mwanaisha

Kanikataa sababu mimi ni Mshona Viatu eee

 

Kampata aaa Mshkaji mwingine ehehe hee hee

Mwenye gari kubwa sana mtumba

Kavunja uchumba mwanaisha sababu mimi ni Mshona Viatu ee

 

(Chorus)

 

[Wote]

Tamaa yako Mwanaisha, itakuponza,
Kwa kumfuata yule bwana mwenye mtumba,
 
Mwanaisha ,Mwanaisha, ogopa sana mamaaaa
kazi ni kazi Mwanaisha , bora mkono uende kinywani eeeh

 

Rudi mwanzo

 

[Ukombozi Africa Urafiki Jazz Band]

Mwenyekitiiiiiii,

Wa nchi tano zilizo mstari wa mbeleeee,

Tunakuomba,  Uzidishe mapambano ya kusini,

Mwa Afrika,

Kwani maadui , wa Afrikaaaaaaaaaa,

Walisumbua sana bara letu hili la Afrika.

 

Raisi Kaunda, na Samora wa Msumbiji,

Silais Khamaaa, wananchi wa Angola ,

Tunawaambiaaaa, Aluta continua

Kibwagizo:

Mwenyekiti Mwalimu Nyerere baba, ( Nyerere baba ),

Imarisha ukombozi wa Afrika ( Afrika ) x2 

Uhuru wetu hauwezi kuwa safi,

Mpaka Afirika yote imekuwa huru Mwalimu eeeeh

Kibwagizo:

Mwenyekiti

Maadui wa Bara la Afirika, wameanza kuwahujumu

Viongozi Mwalimu eeeh

 

Kibwagizo: 

Mwenyekiti ........

Morltara Mohamedi wa Nigeria, na Marien Ngwabi 

Wa Kongo wamepotea Mwalimu eeeh

  Kibwagizo:   

Mwenyekiti .........

[Rudi mwanzo]

 

[Christina - Urafiki Jazz Band ] - tizedboy

Christina e wa mama
Christina ee
Wautesa moyo wangu e Christina e
 
[Mmoja]
Mimi hapa ni kizito sina wasiwasi......tena
Nimejaa sina shaka Christina oo
 
Christina e wa mama....

 

Baba na mama wametuchinjia kuku.....a Christina
Wautesa moyo wangu e Christina e

[Rudi mwanzo]