Ndugu zangu mnaotajwa kwenye ufisadi wa pesa za ESCROW ACCOUNT tuchukue uuamuzi mgumu tupishe wengine nao wasukume gurudumu la Uongozi kwa vile sisi tumeshaonyesha hatuwezi kuendelea. Wale wenzangu na mimi wenye ile idara nyeti jaribuni kuwambiwa hawa wakubwa wetu kwamba huduma yao tena haitakiwi tena, tumeshasikia mengi, tumeshuhudia mengi, tumeyaona mengi sasa itoshe tu kuwa waungwana kama wenzetu wa nchi zilizoendelea kupisha fursa na kuwapa vijiti wengine nao wajaribu.

Haina maana kuendelea kutafuta mbinu na njama za kuzima taarifa ya uchunguzi isisomwe Bungeni wakati ni ninyi hao hao mliokuwa mkijinasibu kwamba fedha hizo si za UMMA. Kama mnao uhakika huo wasiwasi ni wa nini? Mbona tunawaona nanyi mnahudhuria kwenye nyumba za Ibada kama wengine? Kwa nini msiwe na hofu ya MUNGU walau hata kidogo tu? Kwa nini tuendelee kung'ang'ania kana kwamba hakuna wengine wa kuziba nafasi zenu?

Utaalamu wenu umetusaidiaje kwa miaka yote hii wakati umaskini, Ujinga, maradhi na UFISADI ukitamalaki kwa Ari, Nguvu na Kasi mpya?
Jamani mwogopeni Mungu Jamani mwogopeni Mungu.....