Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

Solemba - JUWATA JAZZ(Nico Zengekala)]

 

Ulinipa ahadi tukutane kwenu,

Nikitumaini nimewahi,

Nilichopata kwako ni matusi ooh, ooh na dharau tele

Ungenieleza ukweli solemba,

Kuliko kunidanganya ooh,

Najuta kuitimiza ahadi ooh ambayo si ya kweli.

 

(Chorus)

[Wote]

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,

ila dharau uliweka mbele solemba.

 

[Zengekala]

Nilichomwa na jua toka asubuhi,

mpaka saa nane Solemba sababu ya kukungoja wewe

Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani

Nimeshituka Solemba ,

Nimeshituka Solemba

 

[Wote]

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,

ila dharau uliweka mbele solemba.

 

[Zengekala]

Sikutaki tenaaa, sina haja nawe,nimeshapata mwingine atakaye nipenda kwa roho moja,

Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha kama mimi

Huna huruma Solemba.......Aloi I love you baby

 

[Wote]

Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,

ila dharau uliweka mbele solemba.

 

Rudi mwanzo

 

[TUMA -  Nico Zengekala]

 

Nilisimama kwenye kona, ya uhuru na msimbazi,

Natizama wanaopita , wanaorudi mamaaaa,

Huenda nikaiona sura yake tuma.

 

Nasimama nikiwaza, ahadi yetu tuliopanga,

Tukutane Darisalama, Tuma mama,

Nia na madhumuni wazazi watuone.

Nilishikwa na mnutsuko shoga yake aliniponiejia na kunieleza

 Tuma ee tuma ee keshaolewa

Nilishikwa na mshituko mapigo ya moyo enda mbio

Sikutegemea Tuma, kama angevunja ahadi yetu ama kweli penye uzia hupenyeza rupia 

 

CHORUS:

 

Usinione nimekonda ewe Tuma, hakuna lingine mama

Ila ni wewe Tuma.

(Usiku wote nalala nikikuwaza nakuita jina lako oh oh Tuma)

Repeat: Usinione nimekonda ewe Tuma.

 

Rudi mwanzo