Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoUtalii

Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani zilizojaaliwa kuwa na idadi kubwa ya vivutio vya utalii kuanzia maeneo ya kihistoria (Mapango ya Amboni na mengineyo, Hifadhi ya wanyama ya pori ya Gombe katika mkoa wa Kigoma yenye Sokwe, miji ya Bagamoyo, Kilwa na Zanzibar- mji Mkongwe na nchi ya marashi na viungo), Hifadhi za Taifa (Manyara, Serengeti, Mikumi, Seleous, Ngorongoro) na hifadhi nyingi za wanyama zenye wanyama na ndege wa aina mbalimbali. Milima iliyopo kama vile mlima Meru, na mlima wenye volkano wa Oldonyo Lengai na mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu sana barani Afrika, Kreta ya Ngorongoro na Bonde la Olduvai linalosemekana kuwa ni chimbuko la binadamu wa kwanza.

Tanzania iko katika eneo zuri la kijiografia lenye mwambao mrefu wa pwani kwa ajili ya biashara ya kimataifa (zikiwemo fukwe mpya zinazojitokeza) kwa kuwa inahudumia nchi sita za bara zisizo na bandari. Aidha imezungukwa na maziwa makuu ya Tanganyika, lenye kina kirefu zaidi barani Afrika, Ziwa Victoria ambalo ni miongoni mwa maziwa makubwa duniani- lenye wingi wa samaki wa maji baridi na Ziwa Nyasa lililopakana na Malawi.

Sekta ya utalii ni miongoni mwa sekta zinazokua haraka sana nchini Tanzania na kuongoza kwa kuchangia pato la Taifa (GDP) na pia ni miongoni mwa sekta zinazoongoza katika kuliingizia taifa fedha za kigeni.

Sehemu hii inakupa taarifa zaidi kuhusu Sekta ya Utalii inayosimamiwa na Sera ya Utalii ya Taifa ya Septemba 1999 na sheria tatuSheria ya Hoteli ya 1963, Sheria ya Mawakala wa Utalii (Utoaji wa Leseni) namba 2 ya 1969 na sheria ya Bunge ya mwaka 1992, iliyoanzisha Bodi ya Utalii Tanzania. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-07 10:40:36
Kufaa
3.7
6 Jumla
Inafaa Sana 3
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
2.3
4 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 1
Si Rahisi kabisa 2

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page